Hatua ya 1
Tengeneza Meta App
1. Fungua developers.facebook.com/apps → Bonyeza "Create App".
2. Chagua aina ya app "Business", ipe jina la biashara yako, kisha tengeneza.
3. Ndani ya app, "Add Product" → tafuta "WhatsApp" → bonyeza "Set up".
Mwongozo huu unakupa kila kitu unachohitaji kuunganisha namba yako ya biashara (Meta WhatsApp Cloud API) bila msaada wa mtu yeyote. Muda unaohitaji: dakika ~15.
Akaunti ya Meta Business
business.facebook.com — biashara yako ishaveriwa (verified) ni bora.
Namba ya biashara
Namba isiyotumika kwenye app ya WhatsApp ya simu (namba moja, sehemu moja).
Akaunti ya developer
developers.facebook.com — inatengenezwa bure kwa dakika chache.
Nakili hizi mara moja — utazihitaji kwenye Meta App Dashboard (WhatsApp → Configuration).
https://www.africhati.com/api/webhooks/meta/whatsappwhatsapp-saas-verifyHatua ya 1
1. Fungua developers.facebook.com/apps → Bonyeza "Create App".
2. Chagua aina ya app "Business", ipe jina la biashara yako, kisha tengeneza.
3. Ndani ya app, "Add Product" → tafuta "WhatsApp" → bonyeza "Set up".
Hatua ya 2
Meta App Dashboard → WhatsApp → "API Setup". Hapa utaona sehemu ya identify: nakili "Phone Number ID" (mf. 1478905148636333).
Namba yako ya biashara lazima iwe ndani ya WhatsApp Business Account (WABA) — kama haipo, ongeza kwenye "From" number kwenye ukurasa huo.
NB: WABA ID yenyewe inavutwa na AfriChat kiotomatiki wakati wa kuthibitisha — hauitaji kuiweka.
Hatua ya 3
Token ya "API Setup" inamalizika baada ya saa 24 — ni ya majaribio tu. Kwa uzalishaji, tengeneza tokeni isiyomalizika:
business.facebook.com/settings → "System Users" → "Add" → jina + role "Admin".
Chagua System User wako → "Generate Token" → chagua app yako → weka ruhusa hizi 3: whatsapp_business_messaging, whatsapp_business_management, business_management.
Nakili tokeni (inaanza "EAAG...") na ihifadhi kwa usalama — huioni tena. Kisha ipe System User haki za WABA: Business Settings → System Users → Assets → WhatsApp Accounts.
Hatua ya 4
Ingia kwenye AfriChat → "Miunganisho" → bonyeza "Unganisha Namba".
Jaza: Namba ya kuonyesha (mf. +255 742 000 111), Phone Number ID (kutoka HATUA 2) na Tokeni ya Access (kutoka HATUA 3) — kisha bonyeza "Unganisha".
AfriChat huthibitisha credentials na Meta kwanza (inavuta namba halisi + WABA ID), kisha token inasimbwa AES-256-GCM kabla ya kuhifadhiwa.
Hatua ya 5
Meta App Dashboard → WhatsApp → "Configuration" → bonyeza "Edit" kwenye Webhook.
Weka Callback URL na Verify token (nakili hapo juu) → bonyeza "Verify and save" — Meta itatuma ombi la GET na AfriChat itajibu.
Mwisho, kwenye "Webhook fields" → subscribe "messages" — ndicho channele inayokuletea ujumbe wa wateja kwenye inbox.
Tuma ujumbe wa WhatsApp kwenda namba yako ya biashara (mf. "Habari"). Ujumbe unapaswa kuonekana kwenye "Inbox ya Pamoja" ndani ya sekunde chache. Kwenye "Miunganisho" unaweza pia kutumia kadi ya Diagnostics ("Test token") kuhakiki credentials — na "Matukio ya Webhook" kuona events zinazoingia.
Token haiwahi kavu
Inasimbwa AES-256-GCM na hairudwi kwenye browser kamwe.
Uhakiki wa Meta
Credentials hubadilishwa na Meta kwanza kabla ya kuhifadhiwa.
Webhook iliyosainiwa
Ujumbe wa Meta hubainishwa kwa X-Hub-Signature-256.
Developer wa CRM yako anaweza kupush taarifa zote za duka (bidhaa, bei, stoo, wateja, maarifa) na kuvuta oda zilizoingia kupitia WhatsApp — AI ya AfriChat inatumia data hiyo mara moja kwa kujibu wateja.
Jinsi ya kuanza (dakika 3):
1. Ingia AfriChat → "Zana" → kadi ya "Developer API".
2. Bonyeza "Tengeneza API Key", ipe jina (mf. "CRM ya Duka") — nakili key MARA MOJA (haitaonyeshwa tena).
3. Mpe developer wako key + base URL hii:
https://www.africhati.com/api/public/v1Ukifungua Base URL kwenye browser utaona ukurasa wa taarifa za API — hii ni endpoint ya machine-to-machine, kwa hiyo kusoma/kuandika data kunahitaji API key (siyo kutembelea kama tovuti).
| Kitendo | Kazi |
|---|---|
| GET /ping | Kagua key + tenant (jaribio la kwanza) |
| GET /products | Bidhaa zote za duka (jina, bei, stoo, sku) |
| POST /products | Push/upsert bidhaa kutoka CRM (kwa sku au jina) |
| GET /contacts | Wateja walioingia (WhatsApp/FB/IG/Web) |
| POST /contacts | Push/upsert wateja wa CRM (kwa waId) |
| GET /knowledge | Maarifa ya AI yanayotumika sasa |
| POST /knowledge | Push maarifa ya duka (bei, masaa, ofa, stoo...) |
| GET /orders | Vuta oda zilizoingia (status, malipo, items) |
Mifano ya curl:
1. Kagua key
curl -H "Authorization: Bearer afr_live_xxx" https://www.africhati.com/api/public/v1/ping
2. Push bidhaa kutoka CRM
curl -X POST -H "Authorization: Bearer afr_live_xxx" -H "Content-Type: application/json" \
-d '{"items":[{"sku":"SKU-1","name":"Sukari Mbao 1kg","price":3200,"stock":150,"category":"Chakula"}]}' \
https://www.africhati.com/api/public/v1/products3. Push maarifa (AI inajua mara moja)
curl -X POST -H "Authorization: Bearer afr_live_xxx" -H "Content-Type: application/json" \
-d '{"items":[{"question":"Masaa ya duka","answer":"Tunafungua Jumatatu-Jumamosa 8:00-18:00"}]}' \
https://www.africhati.com/api/public/v1/knowledge4. Vuta oda mpya (kila dakika 5)
curl -H "Authorization: Bearer afr_live_xxx" "https://www.africhati.com/api/public/v1/orders?status=NEW"
Key moja = tenant moja
Key inaona data za workspace hiyohiyo tu — hakuna kuvuka tenanti.
Ombi 60/dakika
Kwa kila key — kikomo kinarudisha 429.
Futa key = koma mara moja
Zana → Developer API → Futa. Hash tu inahifadhiwa kwenye DB.
NB: Plan ya Enterprise pekee ndiyo yenye Public Developer API — mengine (WhatsApp API ya Meta, webhook, widget) zinafanya kazi kwenye plans zote.
Ingia kwenye mfumo, fuata HATUA 4 — na kama ukiwama, timu yetu ipo kwenye WhatsApp.